Jeremiah 46:26-28

26 aNitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana.
27 b“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,
usifadhaike, ee Israeli.
Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali,
uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.
Yakobo atakuwa tena na amani na salama,
wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.

28 cUsiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,
kwa maana mimi niko pamoja nawe,”
asema Bwana.
“Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote
ambayo miongoni mwake nimekutawanya,
sitakuangamiza wewe kabisa.
Nitakurudi, lakini kwa haki tu,
wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”
Copyright information for SwhKC